Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kilifi- Malindi imeshuhudia ongezeko la miili ya wafuasi wa dhehebu tata ya pasta Paul mackenzie.
Kutokea kwa familia za waathiriwa kutafuta miili ya wapendwa wao huku wapelelezi wakiendelea kufukua miili zaidi na kupeleka hospitalini, imedumisha harufu ya kifo na uchungu.
Robert Chonga, afisa anayesimamia hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi, amefichua kuwa chumba cha kuhifadhia maiti kimezidiwa na idadi ya miili kutoka msitu wa Shakahola.
Chonga alieleza kuwa wanatafuta njia mbadala ya kuhifadhi miili iliyofukuliwa kwa heshima ya maiti.
"Hii mortuary kwa kweli imelemewa. Hata hivi tutapata njia mbadala ya kuweza kuhifadhi zile miili. Tunaangalia njia kadhaa kueza kuona njia mwafaka ya kuweka hii miili kwa njia ambayo inaonyesha heshima," Chonga alisema.
- Nipo tayari kufa, Jela mateso – Mchungaji Mackenzie
- Awamu ya pili upasuaji maiti zilizofukuliwa yaanza
- Mackenzie na mkewe wa tatu wakutana kortini
- Paul Makenzie: Mimi na familia yangu tutakua wa mwisho kufa na kwenda mbinguni
- Zoezi ufukuaji miili waliofariki kwa mfungo tata lasitishwa
- Read all related articles