Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mackenzie na mkewe wa tatu wakutana kortini

Screenshot 20230506 074557 Chrome Mackenzie na mkewe wa tatu wakutana kortini

Sat, 6 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhubiri mwenye utata Paul Mackenzie, anayehusishwa na mauaji ya halaiki Shakahola, alikutana kortini na mkewe Rhoda Mumbua Maweu tangu wakamatwe.

Mackenzie anatuhumiwa kutekeleza dini potofu dhidi ya waumini wake, na kusababisha wengi kupoteza maisha baada ya kufunga hadi kufa kwa lengo la kumuona Yesu, kama walivyoahidiwa naye.

Mumbua anatuhumiwa kuhusika na kuwaleta wanachama wapya, na alipatikana na makachero akiwa mafichoni eneo la Mtwapa pamoja na shangazi yake mnamo Mei 1 majira ya usiku.

Hata ingawa wanandoa hao waliketi sako kwa bako, iligundulika kwamba, Mackenzie alimtazama Mumbua kama kwamba hawajuani.

Kulingana na ripoti kadhaa, Mumbua ni mke wa tatu wa Mackenzie, na alizaliwa mwaka wa 1998 na alikuwa mwanafunzi aliyetiwa fora kwenye mtihani wa KCSE 2016.

Inasemekana kwamba mhubiri huyo alikuwa na wake wawili ambo waliaga dunia.

Wanamitandao waliotazama video ya wanadoa hao wakiwa kortini walitoa maoni yafuatayo:

Wanjiru: "He is looking at his wife like 'oooh kimekurambaa."

Fay_bahati: "Pastor Mackenzie anaangalia bibi yake and he's like, 'alaah, hata wewe umefika hapa."

RealBobo: "He was looking at his wife, and he is like 'kumbe we were not just soul mates but also cellmates."

Maggynjuguna: "Anaangalie wife yake kaa customer."

User9052134334160: "Pastor Mackenzie looking at his wife. Be like pia wewe mambo yamekuendea mulama."

Adelide Okello: "He is shocked to see the wife hata karibu he's like kitawaamba."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: