Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Muhudumu wandege aliyekufa kwa njaa ili akutane na Yesu

Betty Ajenta Charles Muhudumu wandege aliyekufa kwa njaa ili akutane na Yesu

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kisa cha Betty Ajenta Charles (pichani), kinasikitisha na kutafakarisha sana. Mwili wake umefukuliwa baada ya kufunga mpaka kufa katika sakata linaloendelea nchini Kenya la Mchungaji Paul McKenzie ambaye anawafungisha waumini wake hadi mauti (Fasting to Death) ili wafike mbinguni kirahisi.

Mwili wake ni kati ya miili zaidi ya 90 iliyofukuliwa katika zoezi linaloendelea kwenye jimbo la Kilifi - kijiji cha Shakahola, Pwani ya Kenya. Marafiki na ndugu za Betty wamepata mshtuko mkubwa.

Betty alikuwa mfanyakazi wa @qatarairways, Shirika kubwa la ndege duniani. Aliamua kuacha kazi, akauza ardhi yake kwa Kshs 7,000,000 = sawa na TZS 121,170,000/= na kumkabidhi Mchungaji Paul McKenzie.

Mtoto wa Betty aitwaye Jason alilazimishwa kufunga kwa muda mrefu bila kula hali iliyopelekea aage dunia. Wakati mtoto huyo anafunga hadi kufariki, Betty alikuwa nchini Qatar. Jason alikuwa akiishi na babu na bibi yake kwa wakati huo. Haijulikani ni nani alimruhusu mtoto huyo kufunga hadi kufa.

Baada ya kupokea taarifa za kifo cha mwanaye, Betty alifunga safari kutoka Qatar hadi Kenya kwa ajili ya mazishi ya mwanae. Baada ya mazishi alipotea na hakujulikana alipo tena.

Dada yake anayeishi eneo la Umoja - Nairobi, anasema Betty aliacha barua ya hisia kali kwa mume wake akionesha asingerejea tena milele. Baada ya kuandika barua hiyo Betty aliondoka na wanae wengine kuelekea kwenye Kanisa la Mchungaji McKenzie katika kijiji cha Shakahola, huko Kilifi, kaunti ya Malindi. Alifuta akaunti zake zote za mitandao ya kijamii, akauza vitu vyake vyote, kabla ya kupanda ndege kuelekea Malindi.

Rafiki yake anasema, Betty alimuaga akimjulisha kuwa anaenda kuonana ana kwa ana na Yesu tar 08 Aprili 2023 huko Malindi na hivyo ataondoka Nairobi tar 07 Aprili 2023. Alipofuatilia aligundua Betty alikata ticket ya ndege ya kwenda tu (one way) na siyo ya kwenda na kurudi (round trip).

Katika msako unaoendelea kwenye eneo la ekari 800 linalomilikiwa na Mchungaji Paul Mackenzie, Polisi wamemkamata Mchungaji mwenza anayejulikana kama "Zablon wa Yesu" akiwa anasoma Biblia akieleza yeye angelianza kufunga Juni 2023. A typical KIBWETERE.!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: