Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahadzabe wasikitika kunyimwa bangi kushiriki sensa

Bangi Pic Data Wahadzabe wasikitika kunyimwa bangi kushiriki sensa

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Wakati Serikali ikitoa nyamapori ya nyumbu 20 kwa jamii ya wawindaji, waokota matunda, wakusanya mizizi na warina asali ya wahadzabe wa bonde la Yaeda Chini Wilayani Mbulu Mkoani Manyara ili wahesabiwe, baadhi yao wamelalamika kunyimwa bangi katika mgawo huo.

Hii ni mara ya pili Wahadzabe hao kutaka wapatiwe nyama pori ili wahesabiwe kwani sensa iliyofanyika mwaka 2014 walitaka wapatiwe nyama ya nyani na bangi ili washiriki sensa ila wakapewa nyama na kunyimwa bangi.

Akizungumza baada ya kupewa nyama hiyo leo Agosti 23, kazi wa mkazi wa Kijiji cha Mongoamono, Malam Dodokhoye amesema japokuwa atashiriki sensa ya watu na makazi na wenzake baada ya kupewa nyama hizo ila wamesikitishwa kunyimwa bangi.

“Tunamshukuru mtoto wa Nyerere kwa kutupatia nyama ya nyumbu ila amekataa tusiletewe bangi, japokuwa tumekubali tutashiriki sensa ya watu na makazi kwa kuhesabiwa huku Yaeda Chini,” amesema Dodokhoye. 

Naye mkazi wa mji mdogo wa Mirerani, Abdi Soka amesema hadi saa tano asubuhi makarani wa sensa walikuwa bado hawajafika kwenye makazi yake hivyo anawasubiri ili ahesabiwe.

Akizungumza na jamii hiyo, Mkuu wa mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere amewataka kushiriki sensa ya watu na makazi kwa mustakabali ya maendeleo kwa serikali kutambua idadi ya wananchi wake.

“Tumesikia kuwa mlitoa masharti kuwa ninyi ni wawindaji na siku ya sensa Agosti 23 mtaenda kuwinda, sasa tumeona tuwape nyamapori nyumbu 20 ili mle nyama na kusubiri makarani wawahesabu,” amesema Makongoro.

Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Hanang’ Janeth Mayanja ameshiriki sensa ya watu na makazi kwa kuhesabiwa kwenye makazi yake mji mdogo wa Katesh.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera ameshiriki sensa ya watu na makazi kwa kuhesabiwa katika makazi yake mji mdogo wa Orkesumet.

Chanzo: Mwananchi
Related Articles: