Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia ahutubia Taifa kuhusu Sensa ya Watu na Makazi, Ikulu Chamwino

Samia Hotuba Sensaaa Rais Samia ahutubia Taifa kuhusu Sensa ya Watu na Makazi, Ikulu Chamwino

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa kuhusu umuhimu wa kujitokeza kwenye shughuli ya uandikishaji wa Sensa ya Watu na Makazi Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Agosti 2022.

Akizungumza wakati wa hotuba yake, Rais Samia amesema taarifa zitakazokusanywa na makarani wa sensa nchi nzima, ni taarifa za siri kwa mujibu wa sheria ya takwimu sura 321.

“Karani wa sensa haruhusiwi kutoa siri ya taarifa alizokusanya katika kaya akifanya hivyo kwa makusudi ni kosa la jinai hivyo hatua za kisheria zinatachukua mkondo wake.

“Sensa ya mwaka huu ina umuhimu wa kipekee kwa vile imeunganisha sensa ya majengo yote nchi nzima kwa ajili ya kufahamu kiwango cha ubora wa makazi ya wananchi wanayoishi.

“Jambo ambalo halijawahi kufanyika hapa nchini, kukamilika kwa zoezi hili kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kuunganisha sensa ya watu na makazi.

“Nataka nitoe indhari, kutokana na ukubwa wa nchi yetu, makarani hawataweza kufikia kaya zote kwa siku moja, wito wangu kwa wananchi ambao hamtafikiwa kesho tarehe 23 kuhakikisha mnatunza kumbukumbu za watu waliolala katika kaya zenu usiku wa Agosti 23 mwaka huu.

“Karani atakapopita azikute na kuziingiza kwenye mfumo wa kukusanyia taarifa na kama kutahitajika ufafanuzi wowote muwe tayari popote mlipo kutoa ushirikianio wa kutosha hata kwa njia ya simu,” amesema Rais Samia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: