Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makongoro akoshwa na maswali ya Sensa, awataka wananchi kutoa ushirikiano

IMG 20220823 133357 303 768x576 RC Makongoro akoshwa na maswali ya Sensa, awataka wananchi kutoa ushirikiano

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere leo tarehe 23 Agosti 2022 ameshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi,akihesabiwa yeye na familia yake katika makazi yao mtaa wa Mrara Mjini Babati.

Akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi hilo, Nyerere ametoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Manyara kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa pindi wanapofika Katika maeneo yao ili waweze kupata taarifa sahihi zitakazoisaidia serikali kupanga vyema maendeleo.

Amesema zoezi la sensa ni wajibu wa kila mtanzania hivyo inapaswa kufanywa kwa uadilifu mkubwa.

Aidha, amesema amefurahishwa na maswali yanayoulizwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambayo yanalenga huduma muhimu za kijamii zinazopatikana katika maeneo ya wananchi ili kuiwezesha serikali kutambua huduma zinazokosekana katika maeneo hayo na uhitaji wake.

Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi limeanza rasmi leo tarehe 23 Agosti 2022 na kuendelea kwa siku sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: