Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kesi ya Mbowe: Inspekta Swila Akana kuwa 'Mpelelezi wa Mchongo'

Kesi Mbowe 2 Pic Kesi ya Mbowe: Inspekta Swila Akana kuwa 'Mpelelezi wa Mchongo'

Wed, 9 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKAGUZI wa Jeshi la Polisi Tanzania, Tumaini Swila, amedai uhamisho wake wa muda kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Temeke kwenda Makao Makuu Ndogo ya Upelelezi Dar es Salaam haukuwa wa kimkakati kwa ajili ya maandalizi ya kesi ya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni waliokuwa makomando wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Inspekta Swila ametoa kauli hiyo jana Jumanne, tarehe 8 Februari 2022, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano jijini Dar ea Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Ni baada ya Wakili wa utetezi, Fredrick Kihwelo, kumuuliza kama atakuwa sahihi akisema uhamisho wake ni wa kimkakati, kwa ajili ya maandalizi ya kesi hiyo namba 16/2021, yenye mashtaka sita ya ugaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: