Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jude Bellingham mchezaji Bora Bundesliga

Jude Bellingham.jpeg Jude Bellingham

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akiwa na umri wa miaka 19 tu, kiungo wa Borussia Dortmund, Jude Bellingham amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa 2022/23 wa ligi kuu Ujerumani #Bundesliga.

Bellingham raia wa England alikuwa nahodha wa Dortmund na kuweka rekodi ya kuwa nahodha mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya klabu hiyo huku akiifungia magoli 14 kwenye michuano yote.

Bellingham ametwaa tuzo hiyo licha ya Dortmund kuukosa ubingwa wa #Bundesliga kwa utofauti wa magoli mbele ya Mabingwa mara 11 mfululizo Bayern Munich.

Nyota huyo anahusishwa na kuondoka klabuni hapo huku klabu ya Real Madrid ikiwa mstari wa mbele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: