Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu maana na Historia ya Sensa ya Watu na Makazi

Xscds Sensa Fahamu maana na Historia ya Sensa ya Watu na Makazi

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sensa ni nini? Ofisi ya Takwimu ya Taifa(NBS) Sensa ya Watu na Makazi inaielezea sensa kuwa ni utaratibu wa kukuasanya, kuchambua, kutathmini, kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu.

Kwamaana nyingine Sensa ni utaratibu wa kupata na kutunza taarifa kuhusu idadi ya watu, makazi au taasisi Fulani katika nchi husika.Pia ni zoezi lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kujua umri, jinsia, mahali wanapoishi, hali ya vizazi na vifo.

Sensa ilianzia wapi? Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania sense ilianza mwaka 1910. Sensa nyinginze zilizofuata zilikuwa ni mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012 baada ya uhuru.

Kwamujibu wa takwimu wa sensa ya watu na makazi ya mwisho ya mwaka 2012, Tanzania ilikuwa na jumla ya watu 44,929,002 ambao kati yao watu 43,625,434 walikuwa ni wa Tanzania bara huku Zanzibar ikiwa na watu 1,303,568. Sensa ya 2022 itakuwa ni sense ya sita kufanyika Tanzania baada ya uhuru.

Lengo la kufanya sensa ni lipi haswa? Kujua idadi ya watu wote na makazi yao ni muhimu katika mipango yote ya kiuchumi, kiutawala pamoja na huduma mbalimbali za kijamii zinazohitajika katika kuinua hali ya maisha ya watu kitaifa.

Kwa kupata takwimu sahihi za watu na makazi husaidia katika kutunga sera, kupanga mipango ya maendeleo na kuboresha utoaji huduma za jamii kwa watanzania ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa uanzishaji na ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo huchagiza maendeleo ya watu.

Mwisho; Sensa ya watu na makazi ni muhimu sana katika kuimarisha na kuboresha uchumi wa nchi na maisha ya watanzania mmoja mmoja kwa kusogezewa karibu huduma za afya, elimu na za uzalishaji mali.

Hivyo basi watanzania wote wanahaki ya kuungana kuhesabiwa kwa kuangalia tija iliyopo katika zoezi hili. Sensa hii ya mwaka 2022 inatazamiwa kufanyika Jumanne Agosti 23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: