Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asakri: Hatukumshuhudia Mbowe Akipanga Ugaidi

Mboweeepicc Data Asakri: Hatukumshuhudia Mbowe Akipanga Ugaidi

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

INSPEKTA Tumaini Swila amedai yeye pamoja na wapelelezi wenzake hawakuwahi kumshuhudia Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa katika kikao cha kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi.

Swila ambaye ni shahidi wa 13 wa Jamhuri alidai hayo jana Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mbele ya Jaji Joackim Tiganga wakati akihojiwa na Wakili wa Utetezi, Nashon Nkungu.

Alidai kupitia ushahidi aliotoa anaweza kusimama kifua mbele kwamba alitenda haki katika kufanya uchunguzi wa kesi hiyo.

Anadai katika kufanya kazi zao za upelelezi waliongozwa na Sheria ya Kuzuia Ugaidi na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Inspekta Swila anadai yeye pamoja na wapelelezi wenzake hawakuwahi kumshuhudia Mbowe akiwa katika kikao cha kupanga kufanya ugaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: