Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga yaanika mkataba wa Kagoma "Tulimnunua kwa sh milioni 30 kabla ya Simba"

Kagoma Saaa Yanga yaanika mkataba wa Kagoma

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasheria wa Yanga Sc, Patrick Saimon ameweka wazi kuwa mpaka sasa Yusuph Kagoma ni mchezaji halali wa Yanga Sc na walimsainisha mkabata wa miaka mitatu na kumtumia hadi tiketi ya ndege kutoka Kigoma nakuja Dar es salaam kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu 2024 - 2025.

“Yanga imeshutumiwa sana kuhusiana na sakata la Yusuph Kagoma, leo kama Yanga tumeamua tuongee kuhusu nafasi ya Yanga Kwenye sakata la Kagoma.

“Ilikuwa Machi 04, 2024 Yanga Sc ilianzisha mchakato rasmi wa maongezi ya kumnunua Kagoma, baada ya maongezi Singida Fountain Gate walifikia muafaka ulitoa kiwango na tukafikia makubaliano ya kulipa milioni 30 ya kumnunua Kagoma.



“Baada ya makubaliano na Singida kuweka Saini, Yanga tulitakiwa kulipa Tsh 15m mwishoni mwa mwezi Aprili na Tsh 15m nyingine mwishoni mwa mwezi Juni, Aprili 30, Yanga tulilipa Tsh 30m ya kumnunua Kagoma na akawa mchezaji halali wa Yanga.

“Machi 27 tulimtumia mchezaji tiketi ya Ndege kutoka Kigoma kuja Dar na alifika klabuni tukafanya nae mazungumzo na tukasaini mkataba na Kagoma na alisaini mkataba akiwa na wakili wake akasaini mkabata wa kuitumikia Yanga miaka kwa mitatu,” Mwanasheria wa Yanga Sc, Saimon Patrick.

"Mpaka sasa tunaongea Yusuph Kagoma ni mchezaji halali wa Yanga Sc tulimsaini miaka mitatu na tukamtumia hadi tiketi ya ndege kutoka Kigoma nakuja Dar es salaam kuungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu 2024 - 2025.

"Baadaye Singida wakatuandikia kuwa ile pesa tuliyowalipa ya Kagoma waihamishie kwenye usajili wa Kibabage, tulikataa na tukawalipa milioni 30 nyingine ya usajili wa Kibabage zikawa milioni 60 kwa jumla.

"Baada ya kukamilisha usajili Kagoma alikuja Yanga akasaini mkataba alkiwa na mwanasheria wake, lakini baadaye akafanya double signing. Baada ya sakata kuwa kubwa uongozi wa mchezaji walituandikia barua kuomba suala hilo tuliondoe kwenye kamati ya TFF sisi tuliwapa sharti la mchezaji aombe radhi hadharani lakini hajafanya hivyo," amesema wakili Patrick Saimon.

Ikumbukwe pia Kagoma amesaini mkataba na klabu ya Simba na tayari Simba walishamtambulisha kama mchezaji wao.



Risiti ya malipo ya klabu ya Yanga kwenda Singida fountain gate iliyolipwa siku ya tarehe 30 mwezi wa nne kuonesha makubaliano ya kumhitaji mchezaji Yusuf Kagoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: