Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge ataka sheria ya kulinda usalama wa wanafunzi kwenye magari

Nancy Nyalusi. Nancy Nyalusi.

Thu, 23 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalum, Nancy Nyalusi ameitaka serikali kutunga sheria ya kulinda usalama wa wanafunzi wanapokuwa kwenye magari kutokana na kuwapo na ongezeko la shule binafsi.

Akiuliza swali kwa Waziri Mkuu, Mbunge huyo amesema ukuaji wa sekta ya elimu na ongezeko la shule binafsi kumesababisha kuongezeka kwa huduma ya usafiri kwa wanafunzi kupitia mabasi maalum jambo ambalo lina athari nyingi hivyo ni muhimu kutungwa sheria hiyo.

Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema zipo sheria za vyombo vya usalama vyote vinavyotumia moto yakiwemo mabasi yanayobeba wanafunzi na kwamba zinatakiwa kufuatwa kwa ajili ya usalama wa abiria wakiwamo watoto.

Amesema kwenye eneo la mabasi ya wanafunzi serikali imeongeza kanuni ambazo zinawabana wamiliki wa shule kuimarisha mabasi yao na yaweze kutambulika.

Amebainisha moja ya kanuni hizo ni lazima dereva awe na sifa ya kuendesha mabasi ya abiria na kubeba wanafunzi, lazima yapakwe rangi ya njano ili popote linapopita lijulikane ni la shule na liwe na maandishi makubwa ubavuni na mbele.

Hata hivyo, amesem lazima basi liwe na walezi wawili wa kiume na kike kwa ajili ya usalama wa watoto inapotokea dharura wapate huduma kulingana na jinsia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: