Rais wa Yanga, Hersi Said amesema wanafuatilia kama mchezaji nyota wa Kaizer Chiefs, Khama Billiat (32) ataongeza mkataba klabuni hapo kwakuwa ni miongoni mwa wachezaji walio kwenye rada yao.
Billiat ambaye ni raia wa Zimbabwe mkataba wake unafikia mwisho msimu huu, amekuwa nje ya uwanja mzunguko wa pili Ligi Kuu nchini humo kutokana na majeraha lakini tayari ameshaanza mazoezi na haijajulikana kama ataweza kucheza mechi ya mwisho ya msimu.
Akihojiwa na kituo cha FARPost, Hersi amesema; "Ukiniuliza mimi ni moja ya wachezaji ninaowakubali, ubora wake ni mkubwa sana. Kwahiyo kwanini kama tukipata nafasi ya kuwa nae?
Makamu wa Rais wa timu hiyo, Arafat Haji pia amesema watajadili kuhusu usajili baada ya msimu kuisha ila nyota huyo yupo kwenye mipango yao.
"Ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ambaye tungependa kuwa naye kwenye timu yetu,"