Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Abissay Stephen amesema kuwa Klabu ya Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika haimanishi kuwa ni timu bora kuliko timu zilizotolewa kwenye mashindano makubwa barani Afrika.
"Yanga kuingia Nusu Fainali haimaanishi wao sasa ni wakubwa barani Afrika, na wala haitoshi kusema kuwa wao wana kalenda nzuri kuliko Simba Kimataifa. Isipokuwa wameweka rekodi ambayo watu ndiyo watawapima kila msimu kwa sasa.
"Hatuwezi kusema Simba wamefanya uzembe kuishia Robo Fainali CAFCL kwa sababu wamekutana na wakubwa kuliko wao kwa ubora na uwekezaji, ingekuwa wametolewa na Rivers tungezungumza hivyo," amesema Abissay Stephen.
Yanga wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya kombe hilo baada ya kuiondoa Rivers United ya Nigeria na sasa watakutana na Marumo gallants ya Afrika Ksuini.
Una maoni gani kuhusu kauli hiyo ya Abissay?