Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuchomoa kipa

Diarra Pic Data Golikipa wa Yanga, Djigui Diarra

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mabosi wa Yanga wanakuna kichwa baada ya kugundua kuwa kuanzia Januari haitakuwa na kipa namba moja wao, Diarra Djigui na fasta wakaamua mapema kuvamia jeshini, ili kubeba kipa anayedaka kwa sifa, huku ikimpigia hesabu pia kipa wa Mbeya City, Haroun Mandanda.

Djigui aliyesaliwa msimu huu kutoka Stade Malien ya kwao Mali, ni mmoja ya makipa watakaoenda katika Fainali za Kombe la Afrika (Afcon) 2022, hivyo Yanga huenda ikabakia na kipa mmoja tu, Erick Johora, huku Ramadhani Kabwili akipigwa chini mapema.

Katika kuhakikisha wanakuwa na kipa mwenye uwezo au anayekaribia ule wa Djigui, wameona wamchomoe jeshini kipa wa Ruvu Shooting, Mohammed Makaka aliyejizolea sifa mbele ya mashabiki kwa uwezo wake ya kudaka, japo timu yake inapoteza mechi uwanjani.

Mbali na Makaka, Yanga inampigia hesabu Mandanda, iwapo kama itamkosa kipa wa Ruvu basi wambebe yeye asaidiane na Johora ambaye amekosa namba mbele ya Djigui anayefahamika kama ‘Screen Protector’ kwa uwezo wake wa kulinda lango.

Kamati ya usajili ya Yanga inapambana kusaka kipa bora kwani ikigfika Januari bila kumnasa kipa mpya inaweza kuwa tabu kwao kwa vile wamesaliwa na Johora sambamba na kipa chipukizi aliyepandishwa kutika timu ya vijana, Yunus Magaigwa.

Mwanaspoti limepenyezewa taarifa za ndani kuwa, timu hiyo ipo kwenye mazungumzo na makipa hao wanaoamini wanaweza kuisaidia timu kipindi Diarra akiwa Fainali za Afrika, nchini Cameroon.

“Diarra hana kipa wa kumpa ushindani, ndio maana tumeingia sokoni kusaka mtu ambaye atakuwa bora langoni hata asipokuwepo yeye na hivi karibuni tunatarajia kukosa huduma yake kwani anatarajia kwenda kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano makubwa,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika ndani ya Yanga.

“Ni mapema sana kukuthibitishi kwamba ni nani atakuwa sahihi ila tayari tumeshaanza mazungumzo na makipa wawili wazawa hatuwezi kutoka nje ya nchini kusaka kipa mwingine tunahitaji kutoka ndani kikubwa ni ubora tu,” alisema.

Chanzo hicho kilisisitiza kuwa dirisha dogo la usajili watalitumia kusajili kipa, yenye uhitaji mkubwa zaidi, huku nafasi nyingine ikiwamo ya winga anayetumia mguu wa kushoto ikiwa kipaumbele kingine kwao.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz
Related Articles: