Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kuanika kikosi kizima Julai 1

Yangasc Kosi Yanga kuanika kikosi kizima Julai 1

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka katika uongozi wa Klabu ya Young Africans zinabainisha kwamba, Julai Mosi, mwaka huu itafahamika rasmi kikosi cha timu hiyo kitakuwaje kuelekea msimu ujao.

Katika kukifahamu rasmi kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao, wachezaji wapya waliosajiliwa, walioongezewa mikataba na wale walioondoka watawekwa wazi.

Julai Mosi ambayo itakuwa Jumatatu ya wiki ijayo, mbali na kujulikana usajili mzima wa kikosi cha timu hiyo, pia itafahamika kambi itakuwa wapi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, amesema: “Julai Mosi ndiyo siku ambayo sisi Yanga tutangaza kambi ya timu yetu itakuwa wapi, pia tutaweka bayana kikosi chetu cha msimu ujao kwa maana ya kuwataja wachezaji walioondoka, walioongeza mikataba na wapya waliosajiliwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: