Kumeibuka mjadala kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya wachambuzi na mashabiki wa soka wakidai kuwa kiwango cha kiungo mshambuliaji wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki kimeporomoka na hatoi kile alichotarajiwa kufanya na Wananchi hao wa Jangwani.
Takwimu za kiungo mshambuliaji Aziz Ki tangu asajiliwe Young Africans mwanzoni mwa msimu huu wa 2022/23 wakiwa na matarajio makubwa kwake kuisaidia klabu hiyo.
Assist vs Simba SC - Ngao
⚽ vs Zalan - CAFCC
⚽ vs Club Africain - CAFCL
⚽ vs Azam - NBC
⚽ vs Mtibwa - NBC
⚽ vs Transit camp
⚽ vs Rhino Rangers - FA
⚽ vs Simba SC - NBC
⚽ vs Mtibwa - NBC
⚽ vs Namungo - NBC
Assist vs Coastal Union - NBC
Assist vs Real Bamako - CAFCC
09 - Magoli aliyofunga
06 - Assists
Aziz Ki ndiye ameipeleka Yanga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa goli lake pekee dhidi ya Club Africain na sasa Yanga iko robo fainali ya Mashindano hayo.
Alisajiliwa kwa kitita cha pesa kisichopungua Tsh milioni 400, ameipeleka Yanga Makundi na hatimaye robo (CAFCC), wamepata Tsh milioni 820 Milioni. Endapo Yanga itafika nusu fainali, itapata Tsh Bilioni 1.2.
Ukitazama magoli yake 80% yalienda moja kwa moja kuamua mchezo.
⚽ vs Mtibwa = Points 03
⚽ vs Africain = Makundi
⚽ vs Azam = Points 03
Assist vs Azam = Points 03
⚽ vs Simba = Point 1
⚽ vs Namungo = Points 03
Assist vs Coastal
Katika msimu wake wa kwanza Tanzania ambao haujakamilika, takwimu za Aziz ni hizo, turudi kwenye swali la msingi, Je, ni kweli amefeli?