Mhsmabuliaji mpya wa Klabu ya Yanga, Hafizi Konkoni amesema kuwa atapambana kuhakikisha anapata nafasi kuitumikia klabu hiyo pamoja na Timu yake ya Taifa ya Ghana.
Konkoni amesema hayo wakati akihojiwa na Yanga TV, Kambini Avic Town na kuongeza kuwa yeye atafanya kazi yake kama Konkini na si kama Mayele kwa sababu Mayele amefanya makubwa ndani ya klabu hiyo na yeye atafanya kwa uwezo wake kufikia malengo ya Klabu.
Konkini (23) amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea Bechem United FC ya Ghana ambayo ameitumikia kwa miaka saba.
"Nitapambana sana Yanga kwa sababu sihitaji kupoteza nafasi kwenye timu ya Taifa ya Ghana (Blck Stars), ninahitaji kocha aendelee kuniita na kunipa nafasi na kuwakilisha Taifa langu, kwa hiyo sio kazi rahisi ninanitaji kujituma sana kwa sababu Ghana ina vipaji vingi vya soka.
"Ninahitaji kufanya makubwa na Yanga kwa sababu ni klabu kubwa ina mashabiki wengi hata kwenye mitandao yangu ya kijamii ninaona japo sifahamu Lugha yao (Kiswahili) lakini matarajio yao kwangu ni makubwa, hivyo nina deni kubwa la kuonyesha zaidi ya nilicho nacho, hivyo wanivumilie," amesema Konkoni.
Mashabiki wengi wa Yanga wanatamani mchezaji huyo awe na uwezo kama Fiston Mayele ambaye ameondoka na kuacha alama kubwa klabuni hapo ambapo kwa misimu miwili amefunga mabao 54 na kuisadia timu yake kubeba mataji 6 ya ikiwemo Ligi Kuu mara mbili na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.