Ukiingia kwenye mitandao haswa kwa wanamichezo trend ni #KeyDay ya mechi ya Yanga ambayo imekua dedicated kwa Aziz Ki.
Yanga inazungumzwa sana, Picha zinapostiwa saana na kila kitu ni Kipensi na Funguo, wameifunika Promo ya Mechi ya Simba kwenye mitandao.
Simba hawatengeneza Promo kubwa kuelekea Mechi dhidi ya Power Dynamos pengine kama nilivyosema, Simba kwa sasa kuingia makundi sio stori ndio maana unaona mashabiki hawana wasi na matokeo wanalilia kucheza vizuri (Boli Litembee). Lakini kwenye mechi hiyo Simba wameenda mbali kwa kutengeneza Element ya Biashara.
Simba wameamua kuweka screen Kubwa kwenye maeneo ya wazi (Fans Zone) ili mashabiki wapate nafasi ya kuonja ladha ya Kuwa pamoja kama uwanjani ambapo ni lengo la kibiashara maana ni sponsorship activation.
Yanga wao wamechagua trend ambayo ni kwenda makundi kwa staili yao bila Sponsorship Activation. Simba kaongeza Thamani kibiashara, Yanga kaongeza Thamani ya Ushabiki.