Watani wa jadi, Simba na Yanga, wana dakika 180 za moto kabla ya kukutana kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 16, mwaka huu.
Ni mechi mbili wanazo mkononi ambapo mchezo wa kwanza kwa kila timu ni hatua ya robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports, kisha kete inayofuata ni ya ligi.
Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa mataji yote hayo mawili, wataanza na Geita Gold Aprili 8 Uwanja wa Azam Complex, kisha kete itakayokamilisha dakika 180 itakuwa ni dhidi ya Kagera Sugar, Aprili 11. Zote nyumbani.
Simba wao hawana taji wanalotetea bali wanapambana kupata mataji hayo, kete yao ijayo ni dhidi ya Ihefu Aprili 7. Wakimalizana hapo keteinayofuata itakuwa ni mchezo wa ligi dhidi ya Ihefu ugenini, Aprili 10.
Baada ya watani hao kumaliza kete hizo mbili, kituo kinachofuata ni mechi yao ya ligi mzunguko wa pili ambapo ule mzunguko wa kwanza walitoshana nguvu kwa kufungana bao