Kuelekea siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi makamu wa Rais wa Yanga, Arafat hajiu amesema kuwa Klabu yao imekusanya jumla ya Tsh bilioni 2 kutokana na viingilio tu kwa msimu uliopita wa mwaka 2022|23.
Haji amesema hayo wakati akihojiwa na Clouds360 ya Clouds TV mapema leo Alhamisi, Julai 20, 2023 jijini Dar es Salaam.
“Viingilio vya uwanjani tumekusanya takribani Tsh bilioni 2 kwa mwaka mzima, ni rekodi ambayo haijawahi kufikia na klabu yoyote hapa nchini, hakuna timu yoyote hapa nchini imewahi kukusanya Tsh bilioni 2 kwa mwaka mmoja kutokana na gate collections.
“Moja ya mchango wa mafanikio ya wiki hii ni mwanzo wa kuchochea kupata fedha kwa ajili ya maboresho ya klanu na kufanya usajili wa wachezaji wazuri, kuihudumia timu vizuri inaposhiriki mashindano ya ndani na nje.
“Safari moja ya kimataifa ili uende ukae hoteli nzuri na upate muda wa kujiandaa unahitajika uwe na angalau dola laki moja, zaidi ya Tsh milioni 200,” amesema Haji.