Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Phillipe Kinzumbi anapoitaka Yanga kuliko TP Mazembe

NM KINZUMBI 344 Phillipe Kinzumbi (kulia)

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Phillipe Kinzumbi ni jina jipya ambalo linagonga kwenye vichwa vya mashabiki wa soka kwa hapa nchini. Jina lake limekuwa maarufu kutokana na kuhusishwa kusajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao.

Kinzumbi kwa mara ya kwanza alionekana akiwa na jezi ya timu yake ya TP Mazembe wakati ambao walikuwa wakicheza dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ukiwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, mechi ambayo alionyesha uwezo wa juu sana.

Sasa baada ya hapo mabosi wa Yanga wakaamua kuvamia nchini DR Congo kwenye mechi ya marudiano na hapo ndipo inatajwa kuwa kila kitu kilikamilishwa kwa ajili ya winga huyo kuhamia Jangwani msimu ujao.

Katika mabosi ambao walienda nchini humo kusimamia usajili huo alikuwepo Ghalibu Said Mohamed ‘GSM’ mwenyewe ambaye ni mmiliki wa kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga.

GSM hakuwa peke yake nchini humo kwani pia walikuwepo Rais wa timu hiyo, Injinia Hersi Said pamoja na Makamu wake, Arafat Haji ambao wote kwa pamoja walikuwepo huko kwa ajili ya timu yao.

Jambo kubwa ambalo Championi Jumatatu linafahamu kuhusiana na uwepo wa mabosi hao ndani ya DR Congo ni kwa ajili ya mambo mawili jambo la kwanza likiwa kwa ajili ya mchezo huo lakini la pili kwa ajili ya kukamilisha dili la winga Kinzumbi.

Kwa upande wa Yanga ni ngumu viongozi kuzungumzia hilo lakini kwa mchezaji mwenyewe imekuwa rahisi kumpata ambapo amefunguka mambo kadhaa kupitia championi Jumatatu kama ifuatavyo ambapo aliyazungumza kabla ya mchezo kucheza dhidi ya Yanga.

MAISHA YA TP MAZEMBE YAPOJE? “Ni maisha halisi ya mpira ambayo kwa mchezaji wa kawaida lazima huyafurahie, unapokuwa mchezaji mkubwa kwa timu za ndani basi lazima hutamani kuichezea TP Mazembe kwa kuwa ni timu kubwa ambayo ina rekodi kubwa sana hapa Afrika.

“Popote Afrika ukienda na kisha ukajitambulisha kuwa wewe ni mchezaji wa TP Mazembe basi lazima utafahamika kwa uharaka zaidi, kuna mengi ambayo naweza kuyazungumza kuhusu TP Mazembe na kisha tukashindwa kuyamaliza.

KWA NINI TP MAZEMBE UNAHISI HAIFANYI VIZURI KWA SASA? “Kuna mambo mengi ambayo yanaendelea lakini unajua kwa mimi ni ngumu kuyasema ni mambo ambayo sio mazuri kuyazungumza mchezaji, mimi natakiwa kuyazungumza yale ya ndani ya uwanja zaidi kuliko haya ya nje ya uwanja zaidi.

“Unajua ni ngumu kuelewa jinsi gani mpira ulivo lakini usione kuwa pengine timu haipati matokeo labda kwa sababu ya kuwa tunaishi maisha magumu hapana huwa inatokea tu kwenye mpira.

“TP Mazembe tunaishi kwenye mazingira mazuri na wachezaji wanafurahia maisha ya timu, kikubwa kwenye mpira mambo kama haya huwa yanatokea, ni kama mpito fulani hivi.

TUMESIKIA YANGA WAPO KATIKA MAZUNGUMZO YA KUKUSAJILI “Ni kweli tayari nimepewa taarifa na uongozi wangu juu ya hili suala lakini kwa sasa mimi siwezi kulizungumzia kwa kuwa nimewaachia wao waweze kumaliza jambo, hili kwani mimi kazi yangu ni kucheza mpira hayo nawaachia viongozi wanaonisimamia mimi na wale wa timu yangu ya TP Mazembe.

UNATAMANI KUICHEZEA YANGA? “Kwa nini nikatae, sidhani kama kuna mchezaji kwa sasa anayecheza Ligi ya DR Congo atakataa kuja kuichezea Yanga, hiyo ni kulingana na ukubwa wa sasa wa Yanga pamoja na malengo yao kwa ujumla, mpira wa Tanzania kwa sasa upo juu.

“Mchezaji akicheza Tanzania kwa sasa basi anapata vitu vingi sana vya tofauti ambavyo havipo katika ligi zetu.

UNAWASILIANA NA WATU GANI PALE YANGA “Kwa upande wa viongozi siwezi kusema watu ninaozungumza nao lakini kwa upande wa wachezaji nawasiliana na wengi kama Djuma Shabani, Yannick Bangala na Lomalisa Mutambala, kwa upande wa wengine kama Tuisila Kisinda na Fiston Mayele wao huwa nasalimiana nao tu lakini hatuna stori nyingi kama hao wengine.

“Mukoko Tonombe anatuelezea sana maisha halisi ya soka la Tanzania, hata yeye anatamani kucheza tena katika ligi hii, hivyo kuna vitu vingi tu kati yetu,” anasema mchezaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: