Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni muda wa Yanga sasa kushusha vyuma vya kimataifa

Eng. Hersi Sdv Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said.

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga chini ya Rais wake Injinia Hersi umebainisha kuwa utafanya usajili wa kishindo katika dirisha kubwa la usajili ambalo limefunguliwa Juni 15 2024.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ina mpago wa kuongeza washambuliaji pamoja na mabeki katika kikosi kwa msimu ujao.

Ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24 wataipeperusha bendera ya Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Wataungana na Azam FC, matajiri wa Dar, huku watani zao Simba wakianguki mashindano ya kombe la shirikisho Afrika.

Ali Kamwe, Afisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua kazi kubwa inapaswa kufanyika ili kupata kikosi bora zaidi jambo ambalo linafanyiwa kazi.

“Tutafanya usajili wa kishindo tunatambua kwamba ili kuwa bora ni muhimu kuwa na kikosi imara jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa umakini mkubwa.

“Kila kitu kipo kwenye mpango kazi na malengo yetu ni kuona kwamba tunakuwa imara kwa ajili ya msimu mpya mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi tunaamini kwamba kazi itakuwa kubwa.” Alisema Ali Kamwe.

Kwa upande wa Injinia Hersi yeye alisema kwamba msimu huu klabu hiyo itafanya usajili wenye lengo kuongeza ushindani na makali kwa msimu ujao, huku akiweka wazi kwamba wachezaji muhimu watabaki na kuongezewa mikataba.

Tayari jambo hilo limfanyika, na mfungaji bora wa klabu hiyo na Ligi kuu kwa ujumla Stephen Aziz Ki, ameongezwa mkataba mwingine na bado ataendelea kuwapa furaha sana Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: