Kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewapa pole mashabiki baada ya kukosa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
Yanga ilishika nafasi ya pili baada ya USM Alger kutwaa ubingwa huo wakishinda kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-2 ambapo walishinda 2-1 ugenini.
Kupitia akaunti yake rasmi ya Instagram ameandika;
"Wananchi poleni sana, nilipenda kuwapatia kombe klabu yangu ya Yanga na Watanzania, lakini mpira muda mwingine una matokeo katiki, napenda kuwashukuru benchi la ufundi kwa kazi yao kubwa na wachezaji wangu ambao wamepambana kama mashujaa. Asante mashabiki kwa sapoti yenu na upendo,"
Yanga tayari imeanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba kocha huyo ambaye tayari msimu huu ameipa Yanga Ngao ya Jamii, Kombe la Ligi Kuu, medali za CAFCC na sasa wanasubiri fainali Kombe la Azam Shirikisho.