Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nabi: Hatutashambulia hovyo, Marumo ni wazuri

AZIZ NA NABII 1 Kocha Nabi

Tue, 9 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Marumo Gallants hautakuwa mwepesi kwani wanakwenda wapinzani wao ni bora na wazuri.

Nabi amesema hay oleo Jumanne, Mei 9, 2023 wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa kesho katika Dimba la Mkapa, jijini Dar es Salaam.

“Tunajua kuwa mechi ya kesho itakuwa ngumu sana kwani wapinzani wetu ni wazuri na ni bora. Nasema ni timu bora kwa sababu wamefika nusu fainali tena kwa kuitoa timu bora ya Pyramids, kwa hiyo tunawaheshimu na hatutawachukulia poa.

“Mashabiki wao wanajua ukiwa nyumbani lazima ushinde, soka haiku hivyo, unapojipanga na kuweka mbinu zako kupambana na aduni, naye anajipanga kupambana na wewe, kwa hiyo utakuwa mchezo mgumu sana.

“Hii haitakuwa mechi ya kushambulia hovyo hovyo ili ufunge, unaweza kujiachia kushambulia kisha mpinzani wako akapata counter attack au mipira ya kupenyeza akakufunga na habari ikawa nyingine tofauti, mechi ni ya mikondo miwili, kwa hiyo tutacheza kwa nidhamu ya hali ya juu.

“Wachezaji wana ari ya juu, tumejiandaa kikamilifu kulingana na tulivyomsoma mpinzani wetu, tupo tayari kupambana, kujituma na kuhakikisha tunapata matokeo nyumbani. Tutacheza kwa akili sana na contentration ya juu.

“Wachezaji wetu wote wako fiti kucheza mechi ya kesho, kasoro Djuma Shabani ambaye hajafanya mazoezi ya jana sababu ya mafua, bado tunamtazama kama tutaweza kumtumia, lakini wengine wote wapo fiti,” amesema Nabi.

Aidha, Nabi amewataka mashabiki kutokata tamaa wakiwa uwanjani, washangilie mwanzo mwisho dakika 90 kama wanavyofanya mashabiki wa timu za Uarabuni kule mbele, hata kama mchezaji akikosea basi wamshangilie ili kumrudisha mchezoni na kumpa sapoti ili ajitume zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: