Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Eliud Mvella amesema kama taifa tunapaswa kuanza kuaanda mshambuliaji wa kati atakaye mrithi mshambuliaji Johh Rafael Bocco.
Aidha, Mvella amesisitiza kuwa mshambuliaji kinda wa Yanga Clement Mzize ndiyo mbadala sahihi wa Bocco.
"Hatuna mchezaji wa kusimama mbele kwa sababu Mbwana Samatta anatakiwa acheze nyuma ya mtu (Inside ten) lakini lazima tuwe na mtu mwenye uwezo, nguvu na uwezo wa kumiliki mpira kama ilivyokuwa Bocco.
"Ni muhimu sana lakini ugonjwa huu utatibika siku si nyingi kama walimu wakikaa na wakamtengeneza yule kijana Clement Mzize wa Yanga. Mimi naamini Yule ndo atakuwa tiba. Lazima TFF wa mwambie mwalimu wa timu ya Taifa," amesema Mvella.