Mshambuliaji Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele anashika nafasi ya pili katika orodha wa wafungaji wa mabao kuelekea mechi za mwisho za hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
Fiston Mayele tayari ana mabao matatu hadi sasa akiwa nyuma ya Mghana, Paul Acquah wa Rivers United ya Nigeria na Aubin Kramo Kouamé wa ASEC ya kwao, Ivory Coast wenye mabao manne kila mmoja.
Tayari Mayele amekwishapa Yanga SC tiketi ya Robo Fainali Ligi ya Kombe la Shirikisho kabla ya mechi za mwisho wiki di hii.
Akizungumza na TanzaniaWeb, Mayele amesema kuwa ana wajibu mkubwa wa kuhakikisha anashirikiana na wachezaji wenzake wa yanga kuipambania nembo ya Klabu hiyo na kufikia mafanikio makubwa kwenye mashindano ya kimataifa.
"Jukumu langu ni kuhakikisha ninaipambania timu ipate ushindi, ikitokea nikawa mfungaji bora ni mafanikio makubwa kwangu na kwa klabu, ninatamani iwe hivyo, lakini ninachoikitazama kwa sasa ni kuhakikisha tunashinda mechi zetu," amesema Mayele.
Mayele ndiye mfungaji anayeongoza pia kwenye orodha ya wafungaji wa Ligi Tanzania mpaka sasa akiwa na mabao 15.
Msimammo wa wafungaji bora wa CAFCC mpaka sasa mechi tano za makundi zimechezwa;
Paul Acquah (Rivers United FC) - 4 Kouame Aubin Kramo (ASEC Mimosas) - 4 Fiston Mayele (Young Africans) bao 3 Mostafa Mohamed (Pyramids FC) -3 Boubacar Traore (Union Sportive Monastirienne) -3 Ranga Piniel Chivaviro (Marumo Gallants) -3 Mpho Mvelase (Marumo Gallants) -2 Nyima Nwagua (Rivers United FC) -2 Ary Papel (Al-Akhdar) -2 Lesiba Nku (Marumo Gallants)- 2.