Mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Kalala Mayele, viungo Yanick bangala na Abubakar Salum ‘Sureboy’ huenda wakauoksa mchezo wa kesho dhidi ya Singida Big Stars.
Hayo yamesemwa na kocha msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze wakati akizungumza na wanahabari mjini Singida kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakapopigwa katika Dimba la Liti.
“Kesho kuna wachezaji ambao tutawakosa, Yanick Bangala ni mgonjwa, hatokuwepo, pia tunaangali Fiston Mayele na Salum Abubakari ‘Sureboy’ hizi siku mbili wanaumwa, inabidi tuwaangalie kwenye mazoezi ya leo na madaktari watatuambia kama wanaweza kutumika.
“Wengine wote wapo tayari kwenye mchezo wa kesho. Wachezaji wote wamesha prove kwamba yeyote aliyepo Yanga anaweza kucheza na kufanya vizuri. Hivyo watakaopewa nafasi ya kucheza kesho tunaamini wataitendea haki nembo ya Yanga,” amesema Kaze.