Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastraika Kagera wamtibua Baraza

Baraza Kageraa Kocha Baraza

Sun, 11 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kagera Sugar juzi iliambulia pointi ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, huku kocha Francis Baraza akiwatupia lawama mastraika kwa kukosa umakini na kuzidi kuiweka timu kwenye hali mbaya tangu ulipoanza msimu Agosti 15.

Kagera ilipata pointi hiyo baada ya sare ya bao 1-1 na Geita Gold ikiwa ni baada ya awali kufungwa mechi mechi mbili mfululizom ikilala kwa Simba 2-0 na kulala 2-1 mbele ya Azam, jambo lililomfanya kocha Baraza kuwaka kwa maelezo mastraika wake wamemuangusha.

Baraza alisema ana kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha kwamba anaimarisha safu ya ushambuliaji ikiongozwa na mzawa Yusufu Mhilu akisaidiana na Hamis Kiiza.

“Tuna mabao mawili tu kwenye mechi tatu na tumepata pointi moja. Tunarudi kwenye uwanja wa nyumbani tutahakikisha tunapambana kusaka pointi tatu ili kurudi mchezoni. Kwa upande wangu kazi yangu ni kuinoa safu ya ushambuliaji iweze kutumia nafasi wanazotengenezewa,” alisema.

“Kwenye mechi zote tatu tumetengeneza nafasi za kufunga umakini mdogo ndio umekuwa ukitukwamisha hivyo nitapambana kuhakikisha naondoa changamoto hiyo haraka ili kujitengezea mazingira mazuri ya kukusanya pointi nyingi mzunguko huu wa kwanza.”

Wakati huohuo Baraza alitumia nafasi hiyo kumuomba kocha wa Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ kuboresha timu yake eneo la kiungo na beki wa kati kabla ya kuanza mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika.

“Geita Gold wana timu nzuri lakini kwa nafasi waliyoipata kuiwakilisha nchi kimataifa wanatakiwa kuwa bora zaidi eneo la ulinzi na nimegundua hawajawa sawa pia kwenye kiungo wanakosa watu wazuri.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: