Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mastaa Yanga wamtibua Kaze, atoa kauli hii

Fdgj Yanga Kaze Kikosi cha timu ya Yanga.

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema hajaridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake licha ya kupata ushindi na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam Sports huku akitoa angalizo zito kwa wachezaji wa timu hiyo kutokana na ratiba ngumu waliokuwa nayo kwa sasa.

Licha ya kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la FA katika mchezo dhidi ya Geita Gold uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Yanga inakabiriwa na mchezo miwili migumu ya ligi ambapo Aprili 11 wanatarajia kucheza na Kagera Sugar.

Kisha Aprili 16 wakitarajia kucheza dhidi ya Simba kabla ya Aprili 23, mwaka huu kuwavaa Rivers United katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza nasi, Kaze alisema kuwa licha ya kupata ushindi lakini hakufurahishwa na kiwango cha wachezaji wake kutokana na kucheza kwenye hali ya nchini iliopelekea kupata ugumu wa kupata matokeo ya ushindi kwenye mchezo huo.

“Haikuwa mechi nzuri kwa sababu kipindi cha kwanza tulicheza chini sana hatukuweza kutengeneza nafasi ya bao, lakini kipindi cha pili tulifanya mabadiliko ya kumuingiza Mayele (Fiston) na kufunga bao moja ambalo limetuvusha  nusu fainali.

“Tumepata ushindi na kusonga mbele lakini binafsi sijaridhishwa na kiwango cha chini cha wachezaji walichokionyesha leo (juzi) ingawa kwa sasa tunarejea kwenye uwanja wa mazoezi kurekebisha na kufanyia kazi makosa yote kuelekea kwenye mechi zetu zijazo kwa sababu tuna ratiba ngumu ndani ya mwezi huu, ” alisema Kaze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: