Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marumo Gallants isichukuliwe poa

Marumo Gallants.jpeg Marumo Gallants isichukuliwe poa

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ni rasmi, Yanga sasa itakutana na timu ya Marumo Gallants inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL).

Yanga imetinga nusu fainali baada ya kuitoa Rivers United ya Nigeria kwa mabao 2-0, huku Marumo ikiitoa Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1.

Yanga isiichukulie poa Marumo kwa sababu hadi kutinga hatua ya nusu fainali kwenye hatua ya makundi ilimaliza kinara kwenye kundi A mbele ya FC Lupopo (DR Congo), USM Alger (Algeria) na Al Akhdar (Libya).

Katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Marumo ilianza kwa kuichapa Al Akhdar 4-1, Saint Eloi Lupopo 2-1, kisha ikafungwa 2-0 na USM Algers, ikalipiza kisasi kwa USM Algeria 2-0 lakini ikaja kufungwa 4-1 na Al Akhdar. Katikamchezo wa mwisho wa kundi A, Marumo iliichapa Saint Lupopo 3-2.

Kwenye mechi sita ambazo Marumo ilicheza katika hatua ya makundi, mechi tatu za nyumbani ilishinda ambazo ni mabao 4-1 dhidi ya Al Akhadar, 2-0 USM Alger na 3-0 Saint Eloi Lupopo, huku ugenini ikifugwa 4-1 na Al Akhdar na 2-0 USM Alger kisha ikaichapa 2-0 Saint Lupopo.

Kwa maana hiyo, Marumo sio timu ya kuchukuliwa poa kwa sababu kwenye hatua ya makundi katika mechi za nyumbani haijapoteza mchezo, hivyo Yanga inabidi itumie vizuri mchezo wa nyumbani kuhakikisha inapata idadi kubwa ya mabao ili iweze kujiweka sehemu salama kwenye mechi ya marudiano ugenini.

Marumo ikiwa nyumbani pia kwenye hatua ya makundi haijawahi kupata ushindi kiduchu, bali ushindi wa 1-0 ikiwa nyumbani iliupata kwenye hatua ya robo fainali dhidi ya Pyramids ambao ni mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza ikiwa ugenidi dhidi ya Pyramid kutoka sare ya bao 1-1.

Timu hiyo hadi inatinga hatua ya nusu fainali ni kama Yanga tu kwani imetoa mfungaji bora kinara ambaye ni Ranga Chivaviro akiwa na mabao matano sawa na Fiston Mayele wa Yanga.

Chivaviro ni mshambuliaji hatari kwenye kikosi chao kama ilivyo kwa Mayele kwa sababu hata kwenye Ligi ya Kuu ya Afrika Kusini ametupia wavuni mabao tisa akicheza mechi 17 na kinara wa mabao akiwa ni Peter Shalulile mwenye mabao 11 katika mechi 19 alizocheza msimu huu.

Upande wa Mayele ndiye kinara wa mabao msimu huu akifunga mabao 16 huku anayemfuatia akiwa ni Moses Phiri wa Simba mwenye mabao 10 sawa na Saido Ntibanzokiza, kwa maana hiyo unaona kwamba Marumo ipo vizuri kwenye kila hiyo muhimu.

Licha ya kwamba ipo nafasi ya tatu (ikiwa ni ile ya 14) kutoka chini kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini na pointi 28, ni wazi kwenye msimamo wa ligi inaonyesha ugumu kwani nafasi ya 13 ipo Moroka Swallows ikiwa na pointi 31, nafasi ya 12 ikiwa ni TS Galaxy na pointi 31 huku ile ya 11 na 10 ni Richards Bay na Amazulu FC zote zikiwa na pointi 32 mtawalia.

Kwa maana hiyo nafasi ambayo ipo Marumo isionekane kama vile ni timu dhaifu, bali ugumu wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini unaifanya iwe hivyo na pia uchanga wake katika mashindano hayo kutokana na kuanzishwa miaka mitatu iliyopita.

Katika Kombe la Shirikisho Afrika, Marumo bado licha ya kuwa na Chivaviro ina Lesiba Nku na Mpho Mvelase wakifunga mabao mawili na Celimpilo Ngema, Joseph Malongoane, Letsie Koapeng, Judas Moseamedi na Sibusiso Sibeko wakifunga bao moja kila mmoja.

Upande wa Yanga nayo licha ya Mayele kufunga mara tano wapo kina Kenneth Musonda aliyefunga mawili, Mudathir Yahya, Farid Mussa, Tuisila Kisinda wakifunga bao moja moja.

Upande wa langoni Marumo yupo kipa Washington Arubi ambaye kwa kwa mujibu wa mtandao wa Aiscore ana sevu 20 huku upande wa kipa Yanga, Diara Djigui akiwa nazo tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: