Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndio mrithi wa Imani Kajula Simba SC, Mfahamu A-Z

Uwayezu Francois.jpeg Francois Regis

Sat, 27 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba Julai 26 imetambulisha rasmi Francois Regis kutoka Rwanda kuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo akirithi mikoba ya Imani Kajula aliyejiuzulu wiki chache zilizopita.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya wakurugenzi ya Simba chini ya Mwenyekiti Mohammed Dewji Julai 26, 2024 imefafanua kuwa Regis ataanza kuhudumu katika nafasi hiyo kuanzia Agosti Mosi.

“Tunapomuaga Mkurugenzi Mtendaji wetu Imani Kajula ambaye alijiuzulu miezi michache iliyopita mwishoni mwa Agosti, ninayo furaha kuujulisha umma kwamba bodi ya wakurugenzi ya Simba Sports Club imemteua Uwayezu Francois Regis kuwa Mkurugenzi Mtendaji wetu mpya kuanzia Agosti Mosi, 2024.”

“Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Imani Kajula, kwa niaba yangu na kwa niaba ya Bodi. Mchango wa thamani wa Imani kwa Simba unaacha alama chanya za maendeleo na mafanikio, ambayo yatakuwa ya juu zaidi kutoka ambapo Simba itaendelea kukua,” imefafanua taarifa hiyo ya Simba

Wasifu wa Regis unaonyesha kuwa ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika uongozi wa michezo na hasa soka.

Amewahi kuwa mtendaji mkuu wa Chama cha Soka Rwanda kwa zaidi ya miaka mitatu, amekuwa makamu mwenyekiti wa klabu ya APR na pia amewahi kuwa mratibu mkuu wa mechi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf).

Ni miongoni mwa waanzilishi wa Chama cha makocha wa soka Rwanda ambacho amewahi kuwa makamu wake wa rais.

Regis pia ana taaluma ya ukocha wa soka akiwa na leseni ngazi B ya umoja wa vyama vya mpira wa miguu Ulaya (Uefa) aliyoipata Ujerumani.

Ni mtaalam wa masuala ya utawala wa biashara akiwa na elimu ngazi ya shahada ya uzamili (Masters) na pia ana cheti cha kimataifa cha utunzaji fedha za umma (IPSAS).

Amewahi kufanya kazi kama mkaguzi mkuu wa ndani wa Rwanda, mkurugenzi wa utawala na fedha na pia mkurugenzi wa uendeshaji wa taasisi tofauti ndani ya Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: