Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hersi: Marumo wajiandae kisaikolojia, Yanga tunataka kushinda kila kitu

ENG. HERSI NA MAYELE Hersi: Marumo wajiandae kisaikolojia, Yanga tunataka kushinda kila kitu

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Ally Said leo asubuhi amefanya mahojiano na kituo cha televisheni ya taifa Afrika Kusini SABC kwenye kipindi cha Morning Live jijini Johannesburg.

Eng. Hersi amesema hayo wakati akizungumzia kuhusu klabu yake ya Yanga na maandalizi kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya marumo Gallants.

"Msimu ulipoanza tulianza na mechi ya Ngao ya jamii ambayo tuliwafunga wapinzani wetu Simba na kuchukua taji hilo, ligi ikaanza na sasa tumechukua ubingwa wa ligi kwa miaka miwili mfululizo.

"Mwanzoni wakati naingia kuingoza timu haikuwa kazi nyepesi, tulikuwa na mpango wa muda mfupi ambapo tunadhaminiwa na GMS, ndiyo ametusaidia kupata pesa ya kusajili wachezaji wazuri, kulipa mishahara na kununua vifaa vya kufundishia.

"Mpango wa muda mrefu tumeshauanza na kwa sasa tunaendelea na mchakato wa mabadiliko ya klabu kimfumo ambapo mfumo huo ukikamilika utakuwa ukiwahusisha zaidi mashabiki hasa katika kuiwezesha timu yao.

"Mashabiki wa Yanga wanataka kila mechi timu yao ishinde, kila kombe tunalopambania tubebe, kwa hiyo unapofanya usajili lazima uhakikishe mchezaji unayemchukua atakusaidia kufikia malengo hayo?

"Ari ya upambanaji kwa wachezaji wetu na benchi la ufundi ni kubwa ndio maana tulimaliza mechi 49 bila kushindwa (ubeaten), hii imetufanya kuvunja rekodi ya Tanzania na Afrika Mashariki na kwa Afrika tunakuwa timu ya nne kufikisha michezo hiyo au zaidi bila kufungwa.

"Kimataifa ni mara ya kwanza kwa Yanga kuingia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, kwa hiyo tuna furaha sana kufika hatua hii. Mchezo wa kwanza wa nusu fainali na Marumo kule kwetu Tanzania tulishinda, kwa hiyo tunaamini hata kesho tutashinda na kusonga mbele," amesema Eng. Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: