Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dickson afunguka A-Z majeraha yake Taifa Stars, anarudi uwanjani lini?

Dick Job BBD Dickson Job

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Taifa Stars, Dickson Job amesimulia mazito juu ya majeraha yake wakati alipotolewa kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Guinea, huku akiwatoa hofu mashabiki wa Yanga anayoitumikia.

Job aliumia dakika ya tisa ya mchezo huo baada ya kugongana na kiungo wa Guinea na kulazimika kutolewa dakika ya 11 nafasi yake ikichukuliwa na Bakari Mwamnyeto.

Akizungumza Job alisema baada ya kukutana na ajalih iyo ndani ya uwanja wakati anatolewa alipata wasiwasi kama hataweza kuona tena kufuatia kushindwa kuona kitu kwa takribani dakika moja.

Job alisema hakuwa anaona kitu mbele hali iliyomshtua ambapo bado hafahamu aligongwa na kitu gani kwenye kichwa chake kiasi cha kupoteza netiweki hadi alipopatiwa huduma ya kwanza.

“Sikuwa naona kitu, kuna rangi ambazo hadi sasa sizitambui zilikuwa zinanijia mbele halafu ilikuwa kama dakika hivi sielewi kitu gani nakiona mbele, kiukweli ilinitisha sana,” alisema Job.

Hata hivyo, Job alisema baada ya matibabu alipotolewa hali yake ilianza kuimarika na macho yake kurudi kwenye ufanisi wake.

Beki huyo ambaye ni nahodha msaidizi wa Yanga, alisema kwa sasa hana wasiwasi na afya yake lakini anaamini yuko sawa kucheza mechi ya klabu yake itakapokuwa ugenini dhidi ya CBE SA katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nipo sawa sasa naona vizuri, mashabiki wasiwe na wasiwasi nitarudi kazini kwenye majukumu yangu, hadi sasa ninavyojisikia naona nitaweza kuwa sehemu ya timu kwenye mechi inayofuata kule Addis Ababa.

Yanga itaumana na CBE keshokutwa Jumamosi kkwenye Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa kabla ya kurudiana nao wikiendi ijayo kuamua timu ya kuvuka kwenda makundi ya michuano hiyo ambayo bingwa wake kwa sasa ni Al Ahly ya Misri iliyotwaa msimu uliopita kwa kuifunga Experance ya Tunisia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: