Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Abissay Stephen amesema kuwa kitendo cha Yanga kuomba mechi yao ya nusu fainali Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Singida BS ambao utapangiwa siku nyingine.
Hii imetokana na Yanga kufuzu kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo gallants, mechi ambazo zitachezwa Mei 10 na 17 hivyo ratiba ingekuwa ngumu kwa Yanga kucheza Mechi ya Ligi Mei 4 - Liti, shirikisho la Azam Mei 7 - Liti, CAFCC Mei 10 kwa Mkapa na CAFCC tena Mei 17 Afrika Kusini.
"Yanga kuomba kusogezwa mbele mchezo wao ni haki, pia ni haki kwa TFF kuwajibu barua hiyo kwa sababu tarehe 4 wanacheza mechi ya ligi dhidi ya Singida Big Stars halafu wapumzike siku 3 wacheze tena mchezo mwingine wa ASFC na tarehe 10 wacheze dhidi ya Marumo Gallants.
"Hii ya Yanga kusogezewa mechi walishawahi kupewa Simba kuelekea mechi yao dhidi Kaizer Chiefs ambapo walisogezewa mchezo wao dhidi ya Coastal Union," amesema Abissay Stephen.
Tayari Young Africans ipo mjini Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao utazikutanisha timu hizo katika Uwanja wa CCM Liti mjini humo.
Mchezi huo utachezwa keshokutwa Alhamis (Mei 04), na ulitarajiwa kufuatiwa na mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania bara ‘ASFC’ ambao rasmi umeahirishwa.