Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, linaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na idara zingine ikiwemo ya afya, ili kupata ukweli wa kifo cha Ester Nyangasi (44), mkazi wa kijiji cha Kibedya Wilayani Gairo kutokana na kuwepo taarifa za utata wa kifo chake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amesema Ester alifikishwa hospitali mei 12 katika hospital ya Wilaya ya Gairo na kupewa rufaa, kisha alirudishwa nyumbani na ilipofika Mei 13, 2023 alifariki njiani akirudishwa tena hospitali Hospitali ya WIlaya Gairo.
Amesema, baada ya kifo hicho Mei 14 marehemu alizikwa kijijini hapo na baada ya siku chache zikaibuka taarifa kua kifo cha marehemu hakikua cha kawaida ndipo Polisi kwa kushirikiana na idara ya afya wakachukua kibali cha Mahakama na kufukua kaburi ili kuchukua sampuli za uchunguzi kubaini malalamiko ya ndugu kuhusu kifo hicho.
Hta hivyo, Kamanda Mkama hajaweka wazi malalamiko ya ndugu ambayo yaliibua utata kwemye jamii hadi kupelekea kufukuliwakwa kaburi na kubainisha kua hadi sasa wanawashikilia watu wawili kwa ajili ya upepelezi kuhusu utata wa kifo hicho.