Nyumba inayomilikiwa na Kanisa Katoliki eneo la Mtanda Kati, Lindi Mjini, imeteketea kwa moto hii leo Juni 20, 2023, kwa kukosa msaada wa haraka wa moto kuzimwa baada ya gari la Jeshi la Zimamoto kudaiwa kuwa ni bovu.
Nyumba inayomilikiwa na Kanisa Katoliki eneo la Mtanda Kati, Lindi Mjini, imeteketea kwa moto hii leo Juni 20, 2023, kwa kukosa msaada wa haraka wa moto kuzimwa baada ya gari la Jeshi la Zimamoto kudaiwa kuwa ni bovu. Moto ambao mpaka sasa chanzo chake hakijafahamika umeteketeza nyumba hiyo bila chochote kuokolewa huku wananchi wakidai zimamoto wamekawia kufika na hata walipofika hawakuweza kufanya chochote kwa kuwa gari lao lilikuwa bovu.