Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Tamabu, Alex Lameck (18) Mkazi wa Mission Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya hiyo na kusomewa shtaka la kujeruhi namba 114 la mwaka huu.
Alex anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 225 cha Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 toleo la mwaka 2022.
Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Evod Kisoka, Wakili wa Serikali, Morice Mtoi amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo 25. 09. 2023 katika shule ya Sekondari Tamabu kwa kumjeruhi kwa panga kichwani Stanford Mgaya (37) ambaye ni mwalimu katika shule hiyo.
Mshtakiwa amekana shtaka hilo na amedhaminiwa baada ya kutimiza vigezo vya dhamana na shtaka hilo limeahirishwa mpaka 11. 10. 2023 kwa ajili ya kusoma hoja za awali.