Mkuu wa wilaya ya Njombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Kissa Kasongwa ametangaza vita kwa mwananchi yeyote atakayetekeleza mauaji kwa sababu mbambali ikiwemo migogoro ya ardhi wilayani humo.
Bi Kasongwa amesema tamaduni ya kuuana wilayani humo iwe mwisho kwa kuwa kuna mauaji ya kikatili hali inayoweza kusababisha watu wengine kuogopa kufika katika wilaya hiyo.
“Tamaduni ya kuuana Njombe iwe mwisho, tumuombe Mungu atakase roho ya umauti inayozunguka kwenye hii wilaya ya Njombe,”alisema Bi Kasongwa.
Mkuu huyo wa wilaya, amebainisha hayo wakati akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo katika kata ya Iwungilo yenye lengo la kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.