Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu wa miaka 81 adaiwa kumbaka mtoto kwa ubuyu

Ubuyu (14).jpeg Babu wa miaka 81 adaiwa kumbaka mtoto kwa ubuyu

Fri, 5 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mzee Katembo Mnubi maarufu kama Wajanga mwenye umri wa miaka 81, amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Musoma kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 11 anayesoma katika moja ya shule ya msingi iliyopo Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Akisoma hati ya mashtaka Mwendesha Mashitaka wa serikali Beatrice Mgumba mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya Musoma Alistide Tarimo, mwendesha mashtaka amesema mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya jinai namba 16ya mwaka 2023.

Mwendesha mashtaka aliambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiw hiyo alitenda kosa hilo mara tatu kwa nyakati tofauti kuanzia mwezi wa pili mwaka huu ambapo alikuwa akimuita mtoto huyo kwa kumpatia pesa.

Mgumba ameendelea kuiambia mahakama hiyo kuwa mnamo mwezi Februari mshtakiwa huyo alimuita mtoto huyo kumpatia ubuyu na shilingi 100 kisha mara ya pili alimdanganya mtoto huyo kwa kumwambia aende ndani mwake akachukue hela akamnunulie sigara ndio mtoto huyo alipoingia ndani alimbaka na kumpatia kiasi cha shilingi mia moja.

Mwenshesha Mashtaka wa serikali ameendelea kuiambia Mahakama hiyo kuwa mnamo Machi 2 mwaka huu mshtakiwa huyo alimuita mtoto huyo wakati akiwa anacheza na wezanke shuleni na kumwambia akampikie ugali lakini mtoto huyo alimwambia hajui kupika.

Ila mshitakiwa huyo akamwambia utapika tu hivyo hivyo kisha mtoto huyo akaenda na baada ya kumaliza kupika, mshtakiwa huyo akatimiza azima yake ya kumbaka tena huku akimtishia mtoto huyo kwa kisu na kumwambia endapo atamwambia mtu ana dawa ambazo atajua kama amesema.

Aidha Mwendesha Mashtaka amesema kuwa baada ya kuchelewa kurudi shuleni mwalimu alihoji wanafunzi wenzie kuhusu mtoto huyo ndio wanafunzi hao wakasema alipo na kisha wakamfuata na alipohojiwa na mwalimu akasema kuwa mzee huyo alikuwa akimfanyia kitendo hicho cha ubakaji mara kadhaa na mwalimu akatoa taarifa na kufanikisha kukamatwa kwa mshtakiwa huyo.

Kwa upande wake Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya Musoma Alistide Tarimo, amesema kuwa kesi huyo ipo katika hatua ya kusikilizwa ambapo mashahidi watatu wameishatoa ushahidi wao.

Tarimo ameongeza kuwa washtakiwa wengine watatu wanategemea kutoa ushahidi wao dhidi ya kesi huyo mnamo tarehe 17 mwezi huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: