Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya kutumbuliwa, Mgumba amshukuru Rais Samia

Mgumbaaaaaaaaaa Omary Mgumba

Thu, 2 Mar 2023 Chanzo: Mwananchi

Ikiwa ni siku kadhaa tangu uteuzi wake kutenguliwa kama Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesemshukuru Rais kwa kuiheshimisha familia yake na kuifanya kuwa na historia ya kutoa kiongozi.

Pia amemshukuru kwa kumvumilia kwa kipindi chote cha uongozi wake hadi hapo uteuzi wake ulitenguliwa.

Mgumba aliyasema hayo wakati Akizungumza jana Machi 1, 2023,  Mgumba aliyewahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Songwe kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Tanga miezi miezi saba iliyopita, ameshukuru kuwa miongoni mwa walioaminiwa na Rais Samia na kufanya nyae kazi tangu akiwa Makamu wa Rais hadi sasa.

Rais Samia akiwa Makamu wa Rais, Mgumba alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo kabla ya kuaminiwa na kupelekwa kuwa mkuu wa mkoa wa Songwe na Rais Samia.

“Tunashukuru kwa kuiheshimisha familia yangu na kuwa na historia ya kutoa kiongozi aliyeaminiwa kati ya watu zaidi ya milioni 60.

Namshukuru kwa kunivumilia muda wote hadi jana (juzi). Kila mtu huwa ana hulka na mimi kama kiongozi huenda nilikuwa na hulka zangu ambazo sizioni ila watu wa nje na pembeni walikuwa wanaziona,” amesema.

Amesema sasa maisha yake yataendelea kama kawaida huku akimtaka kiongozi aliyeteuliwa kusimamia maagizo waliyopewa na kuendeleza maono ya Rais Samia katika mkoa wa Tanga.

Mgumba ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, amemtaka mkuu wa mkoa mpya kuhakikisha ndoto za kuifungua Tanga zinaendelezwa sambamba na zile za kuifanya Horohoro kuwa lango la biashara na kusimamia uanzishwaji masoko.

Wakati Mgumba akiyasema hayo, wakazi wa Mkoa wa Tanga wamemtaka Mkuu mpya wa mkoa mpya, Waziri Kindamba kupambana na biashara ya magendo, dawa za kulevya na kuiwezesha sekta ya elimu kuwa katika ubora wake.

Mwanamkuu Hassan wa Duga wilayani Mkinga amesema mkuu wa mkoa wanayemtaka ni yule atakayekomesha magendo kwa kuziba mianya katika njia za magendo za mpakani na nchi jirani lakini pia bandari bubu.

Naye Bakari Rashid wa Kange jijini Tanga amesema angependa kuona mkuu mpya wa Mkoa wa Tanga anatatua migogoro sugu ya ardhi kwa haraka zaidi ili wahanga wa tatizo hilo wapate muda wa kufanya shughuli zao za maendeleo badala ya kuhangaika kila siku kudai haki ya kupokonywa ardhi.

Kuhusu Waziri mpya wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega, wamesema anakabiliwa na changamoto ya kusaidia kupatikana soko la nje la uhakika la dagaa wa baharini (uono) ambao wanaofaidika siyo wavuvi bali ni watu wa kati.

Chanzo: Mwananchi
Related Articles: