Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Mpango kumwakilisha Rais Samia SADC

Mpango Chucrhhh Dkt. Mpango kumwakilisha Rais Samia SADC

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Utatu wa Asasi mbili za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika Lusaka, Zambia Machi 23, 2024.

Makamu wa Rais ataondoka nchini Machi 22, 2024 kushiriki Mkutano huo ambao agenda kubwa ni hali ya ulinzi na usalama katika nchi za SADC, hususan katika Jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mkutano huo utatanguliwa na Mikutano ya maandalizi ya ngazi za Wataalam ambayo ilianza tarehe 17 Machi 2024 na itakamilishwa na Mikutano ya Makatibu Wakuu na Mawaziri itakayofanyika Machi 22, 2024.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ataungana na Mawaziri wenzake kutoka nchi wanachama katika Mkutano huo muhimu. Tanzania kama mwanachama wa SADC na ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani katika nchi za Msumbiji na DRC inashiriki kikamilifu katika ngazi zote za Mkutano huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: