Mwanamke maarufu jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la Swalha ambaye alikuwa anajishughulisha na masuala ya urembo jijini humo, ameuawa kwa kupigwa na risasi na mumewe usiku wa kumkia jana Jumapili ya May 29. Tukio hilo limetokea nyumbani kwa wanandoa hao huko Buswelu.
Taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu wa marehemu akiwa msibani nyumbani kwao marehemu huko Kirumba jijini humo, zimedai kuwa mume wa Swalha anayejulikana kwa jina la Said alichukua uamuzi huo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Amesema Swalha alienda kuangalia mpira na akachelewa kurejea nyumbani. Mumewe hakufurahishwa na kitendo cha mkewe kuchelewa kurudi nyumbani hivyo kukazuka ugomvi baina yao hali iliyopelekea mume wa Swalha kumfyatulia risasi.
Rafiki huyo wa karibu amesema Swalha alifikwa na umauti pale pale baada ya kupigwa na risasi saba za kichwa.