Baadhi ya wananchi wasio na vyama pamoja wale wa CCM wamelalamikia hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Nyasa na mkoa wa Njombe kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliwa halmashauri ya mji wa Njombe
Wakizungumza mbele ya Uongozi wa Wakala wa maji vijijini Ruwasa wilaya ya Njombe na viongozi ngazi ya kijiji na Kata ya Iwungilo waliofika kusikiliza malalamiko hayo wanasema hawakukubaliana nani atauzindua walishangaa kuona Chadema wanauzindua pasina makubaliano ya pande zote
Wakati wananchi wakigawanyika mtendaji wa kijiji cha Uliwa Stunisius Mlowe na mwenyekiti nao wameshangazwa na kitendo hicho ambapo wanasema hawakuwa na taarifa
Kufuatia chama cha demokrasia na maendeleo kupewa heshima ya kuzindua mradi huo na baadhi ya wananchi wa kitongoji cha CANADA na Itowa, Mchungaji Peter Msigwa siku chache zilizopita wakati akizindua mradi huo alisema wananchi wamefanya jambo ambalo ilikuwa lifanywe na serikali na kisha kuchangia fedha kiasi cha lakinane.
Maofisa wa wakala wa maji na usafi wa mazingira mijini na vijijini TARURA wilaya ya Njombe wamefika kijijini hapo na kuwatoa hofu wananchi huku wakisema wanakwenda kuboresha zaidi ili unufaishe watu wengi
Kwa mujibu wa wananchi wanasema walichukua uamuzi wa kujenga mradi huo kwa ngvu zao baada ya kuona serikali imewachangisha fedha kwa miaka mingi lakini maji hayafiki.