Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheria ya uchaguzi itafunuliwa kabla ya uchaguzi - Kinana

Kinana Pic2 Data Abdulrahman Kinana.

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana amesema demokrasia nchini imekuwa na kuna mchakato unafanywa wa kurekebisha sheria zinazohusu uchaguzi kwa ajili ya kuwa na uchaguzi huru na haki wakati mchakato wa katiba mpya unaendelea.

Kinana ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 22, 2023 katika mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, vitongoji na Uchaguzi Mkuu 2025 ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

“Kuna hili jambo linalozungumzwa kuhusu katiba na umuhimu wake, kumekuwa na juhudi nyingi ikiwemo kuunda tume kadhaa, matokeo ya tume hizi baadhi ya mambo yametekelezwa na baadhi bado.

“Hivi karibuni kulikuwa na mchakato wa kuukwamua mchakato Katiba Mpya… kwa sasa hivi kwa kadri ninavyoelewa kuna michakato ya aina mbili; wa kwanza wa kutafuta namna ya kupata katiba ambao unaweza kuchukua muda lakini mchakato wa pili utakuwa wa kurekebisha maeneo yanayohusu uchaguzi na huu unahusu uchaguzi wa 2024 na 2025.

“Sheria inayohusu tume ya uchaguzi, sheria inayohusu namna vyama vya siasa vitakavyosimamiwa, mimi naamini zote zikikaguliwa na zikapelekwa bungeni naamini tutakuwa na uchaguzi huru na haki,” amesema Kinana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: