Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samia awachomolea CHADEMA sakata la kina Mdee na wenzake

Wakipotosha, Toeni Majibu Haraka Rais Samia Samia awakana CHADEMA sakata la wabunge 19 'Sio rahisi jambo lile'

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametolea majibu sakata la CHADEMA na Wabunge 19 wanaohusishwa na chama hicho kuwakilisha sehemu ya viti maalum ya chama ilihali wamekwisha vuliwa uanachama na kusema kuwa kwasasa sio rahisi kwani suala hilo tayari lipo Mahakamani.

Akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimatifa ya Wanawake Dunia ambayo yanafanywa na Baraza la Wanawake Chadema BAWACHA mapema 08, Machi 2023 Mkoni Kilimanjaro, amesema kuwa licha ya kuwa yeye ndiye Rais lakini hawezi kuingilia kila jambo hivyo ni vyema kuacha chombo husika mabacho ni Mahakama kumaliza jambo hilo kisheria.

"Lakini lile la mwisho kwa jina lile mlililoliita na wote wawili wamesema kuwa japo lipo Mahakamani lakini mama lakini mama.... naomba niwambie tuachie mkondo ule uendelee, sio rahisi kutia mkono huko hata kama mimi ni Rais, tuangalie yanayokuja.... CCM oyeeeeee" Amesema Kiongozi huyo Mkuu wa Nchi.

Marejeo haya yanafikiwa mara baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho Freema Mbowe kumuomba Rais Samia kuonea huruma kodi za wananchi zinazotumika kuwalipa mishahara wabunge hao 19 ambao wapo ndnai ya Bunge kinyume na taratibu kwani sio wanachama halali wa CHADEMA

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: