Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji akipigwa, anayelengwa ni kondoo - Lulandala, CCM

Lulandala Ccmd.jpeg Mchungaji akipigwa, anayelengwa ni kondoo - Lulandala, CCM

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Fakii Raphael Lulandala (MNEC), amesema Umoja wa Vijana wa CCM unalo jukumu la kuilinda CCM na Viongozi wake kwa wivu mkubwa bila kuogopa Mtu yoyote ambapo amesema Mchungaji akipigwa anayelengwa ni kondoo.

Ameyasema hayo wakati akihutubia Wananchi Mkoani Dodoma baada ya mapokezi yake yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya UVCCM Dodoma jana Oktoba, 2023 ambapo pia amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVVCM, Kenan Kihongosi.

"Kutakuwa hakuna sababu ya kuwa na Katibu wa UVCCM kwenye Wilaya zetu, kata zetu na Mikoa kama Chama cha Mapinduzi kinashambuliwa katika maeneo yao, ukiona Mchungaji wa kondoo amepigwa lengo sio Mchungaji ni kondoo"

“Suala la kupambana na hoja za Wapotoshaji na Walaghai ni agenda ya kudumu ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: