Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makonda: Bado kuna mengi ya kujifunza

Makonda Paul Ccm Ms Paul Makonda.

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, leo amepokelewa rasmi katika ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam baada ya kuteuliwa siku kadhaa zilizopita.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda amesema ni mapema sana kwa yeye kuanza kuzungumza kwa sababu bado yapo mambo mengi anayopaswa kujifunza kwanza.

Amesema atashirikiana na viongozi na wanachama wote, kuhakikisha CCM inapata ushindi siyo kwenye chaguzi za 2024 na 2025 pekee, bali katika chaguzi zote zitakazokuja.

"Nitumie fursa hii kuwaomba watendaji na watumishi ushirikiano na kunifundisha, kunielekeza na kunishauri kwa uaminifu mkubwa ya kwamba taarifa mnazonipa ndiyo halisi hata wewe ungeifanyia kazi," amesema Paul Makonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: