Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo, amewataka Watanzania kusimama kwa umoja katika masuala ya msingi kwa nchi, akisisitiza wawapuuze wote wanaoeneza maneno ya upotoshaji kuhusu suala la Mkataba wa Ushirikiano wa Kijamii na Kiuchumi kati ya Serikali za Tanzania na Dubai.
Amesema pamoja na Serikali kupaswa kuendeleza utaratibu mzuri wa kuwasikiliza wananchi, pia wananchi wanatakiwa kuisikiliza Serikali hususan kupitia wataalam wake, hasa kwenye masuala yanayohusu utaalam ambapo wananchi wanahitaji kuyajua kwa kusikiliza vizuri, badala ya kufuata maneno ya wapotoshaji.
Amesema, “narudia tena kwamba… pamoja na serikali inapaswa kuendeleza tabia ya kuwasikiliza wananchi, lakini pia wananchi nao wanapaswa kusikiliza Serikali…wanapaswa kuwasikiliza wataalam. Isiwe tu ni one way trafick.”
“Ni lazima Watanzania tuwe wamoja, tusimame pamoja kwenye masuala ya msingi yanayohusu nchi. Puuzeni maneno ya wapotoshaji,” amesema Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Chongolo.