Mfanyabiashara na Meneja wa wasanii mbalimbali Bongo, Rich One amekanusha taarifa iliyotolewa na supastaa wa Bongo Fleva kuhusu tuhuma utapeli anaodaiwa kuufanya msanii Timbulo kwa kutumia jina la Kiba.
Alikiba siku ya Miaka 20 ya Mfalme wikiendi iliyopita alisema kwamba Timbulo aliwahi kuchukua pesa ya shoo ya Alikiba miaka ya nyumba, akawadanganya mashabiki kuwa yeye ni Kiba, kwa mujibu wa Rich One amefunguka kuwa sio kitu cha kweli.
"Kaeni mkielewa kuwa kati ya Timbulo na Alikiba ni Timbulo ndiye aliyeanza kutoka kumuziki, sasa iweje leo Alikiba aje kusimama aseme Timbulo kajifanya Alikiba kwenye shoo.
"Timbulo alianza kubadili nyimbo za nje kuzifanya kwa Kiswahili na zikfanya vizuri akawa mkubwa, Alikiba kaongea upuuzi," amesema Rich One.